MTANGAZAJI

NINI KIFANYIKE KUEPUSHA AJALI ZA BARABARANI TANZANIA???

Mtoto Rukia Haji (2) akinyweshwa maji na mama yake Hawa Rashidi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kupata ajali katika eneo la Maguha katika wilaya ya Kilosa iliyohusisha basi la Scanlik na basi la Al- Hushum
Mmoja wa Majeruhi katika ajili iliyohusisha basi la Scanlik na basi la Al- Hushum akipatiwa huduma ya kwanza na mmoja wa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya kupata jali wakati wakisafiri

Basi la Scanlik linavyooneka baada ya kupata ajali eneo la Maguha mkoani Morogoro.


Basi la Al-Hushum likisukumwa kutoka katika eneo la ajali iliyohusisha basi hilo na nasi la Scanlik katika eneo la Mahuga kilometa 80 kutoka Morogoro mjini ajali hiyo ilitokea jana. (Picha zote na Juma Mtanda)

Hivi ni mpaka lini abiria wataendelea kupoteza maisha yao barabarani ????
Utafiti unaonyesha kuwa hapa nchini zaidi ya asilimia 60 hubaki na ulemavu wa kudumu na wastani gharama za kumhudumia majeruhi mmoja hukadiriwa kuwa sh 700,000 na matibabu yake huchukua wastani wa miezi sita.
mwaka 2005 kulikuwa na ajali 16,388 mwaka 2006 ajali 17,677 na ambapo mwaka 2006, Tanzania ililipoteza jumla ya sh bilioni 508 sawa na asilimia 3.4 ya pato la taifa, kiasi ambacho ni kikubwa katika nchi changa na masikini kama Tanzania.
Uendeshaji wa magari mabovu yasiyokidhi viwango vya ubora husababisha ajali kwa asilimia 16.3 wakati ubovu wa miundombinu na mazingira ya ajali huchangia asilimia 7.3.

Tatizo li wapi na nini kifanyike??

5 comments

Anonymous said...

pole kwa majeruhi..jamani jamani...bongo hatufiki...

Anonymous said...

Hii ni kwa sababu hakuna raisi Tanzania. Kama yupo anafurahia vifo vya wananchi hao. Mfano mzuri ni jinsi ambavyo serikali yake ilishidwa kusimamia adhabu aliyopewa dereva aliyesababisha ajali na vifo vingi, na hatima yake ni kwa madereva WAPUMBAVU, kujidai wanatia mgomo. This is bull shit.

Mzee wa Taratibu said...

Madereva wawekewe ngumu sana kila siku tunasoma ajali za mabasi wanakufa watu bila sababu si uzuri, na sisi tunaogopa hata kuja TZ na kupanda mabasi.

Anonymous said...

Hatari kweli kweli, na pole za wote walio athirika na ajali hapa nyumbani Tanzania, ooo Dr Kikuli Mungu ambariki kwa kazi yake nzuri hapo hospitali ya mkoa wa Morogoro

mdau wa usafirishaji said...

hey hey mdau..tuwie radhi...sisi wa Tanzania tunae Raisi....JK...tatizo sio yeye, tatizo ni la madereva..kwanza tukubali madereva wetu ni mbumbumbu!!!!!!!!!! wengi wa madereva wetu wankimbili kuendesha mabasi ili kujipatia ridhiki na hawaichukulii hiyo kma ni kazi ambayo inahitaji uangalifu mkubwa...unajua mtu ukijijali wewe kwanza hakika utawakumbuka na wengine...pia urimbukeni ndio tatizo.....madereva wetu wakijali kazi zao mambo yatkuwa mazuri tu...pia tatizo lingine ni shuleeeeeeeeeeeeee

Mtazamo News . Powered by Blogger.