MTANGAZAJI

SIKU YA MTOTO AFRIKA

Mtoto huyu baada ya miaka 10 atakuwaje? picha kutoka www.kidskillingkids.blogspot.com

Watoto Wengi wamekuwa wakilazimishwa kujiunga na majeshi.
Jana ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ikiwa na ujumbe wa mwaka huu wa Afrika imfaayo mtoto- "Linda Haki ya Mtoto Kuishi".
Maendeleo na haki za watoto zinapaswa kutekelezwa mahali popote duniani japo kutofahamika kwa haki hizo ama kukikukwa kwazo kunasababisha watoto wengi kunyanyaswa na kuonewa katika jamii.
Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF linaeleza katika tawimu zake zilizotolewa mwaka 2008 kuwa inakadiliwa zaidi ya watoto milioni 300 duniani wamekuwa wakinyanyasika kutonakana na vita,kufanyishwa kazi kwa nguvu na kulazimishwa kufanya mapenzi.

Unyanyaswaji mwingine ni kufanyakazi katika sehemu mbalimbali kama vile shuleni,vyuoni,katika taasisi mbalimbali na kulazimishwa kujiunga katika majeshi ya nchi mbalimbali kuliko na migogoro ya kisiasa, kukeketwa na kulazimishwa kuolewa katika umri mdogo.
Kiasi cha watoto bilioni 1.5 kutoka katika theruthi mbili ya watoto wote duniani wanaishi katika nchi 42 zilizoko katika mapigano ya vita kutokana na migogoro ya kisiasa kati ya mwaka 2002 na 2006 japo imekuwa ni changamoto kupata takwimu za mara kwa mara kutokana na mapigano hayo.
Inakadiriwa kwamba kuna wakimbizi milioni 14.2 duniani ambapo aslimia 41 kati ya hao inaaminika kuwa ni watoto wenye umri chini ya miaka 18,pia kuna watu milioni 24.5 waliathirika na migogoro nchini mwao,ambapo kati yao asilimia 36 ni watoto.

Kwa kuwa uwezekano wa kupata takwimu sahihi kuhusu watoto wakimbizi ambao wamekuwa wakilazimishwa kupigana katika nchi mbalimbali inasemekana kuwa kuna watoto zaidi ya laki moja wamekuwa wakihusishwa kujiingika katika kupigana vita tangu mwaka 1998 ambapo kuna watu milioni 39 ni wakimbizi duniani .

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.