MTANGAZAJI

PASTOR BROWN


Kwa muda wa miaka isiyopungua mitano nimefahamiana na Mhubiri wa kimataifa aliyeko Tampa,Florida nchini Marekani Mch.Moises Brown(pichani akiwa na mkewe),Mpendwa msikilizaji mchungaji huyu ambaye hamfahamu baba yake kutokana na mama yake kumzaa baada ya kufanyiwa kitendo cha kinyama cha kunyanyaswa kijinsia(kubakwa),Historia hii ya aibu na machungu ambayo Mch Brown huisimulia kwa uchungu na niliisikia akisimulia mwenyewe kwenye mkanda wa video ya nyimbo iliyotolewa na VOP.
Hali hii imekuwa ikimgusa sana maishani mjumbe huyu ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili akiwa tayali ana albamu mbili mkononi kwa kuanzisha mpango wa kuwahudumia watoto yatima kule nchini Marekani kwa maelezo zaidi waweza tembelea hapa: http://www.feedourchildren.org/ Kwangu mimi hii naiona ni changamoto kubwa maana baadhi yetu tunafungua vituo vya kuwatunza na kuwahudumia watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu si kwa kukuguswa bali kwa manufaa binafsi hata hao watoto alionao juu si watoto wake wa kuzaa bali anawachukulia kama watoto wake halisi wa kuzaa.
Pr Brown amewahi kuhubiri katika nchi mbalimbali ikiwemo Kenya,Philippines,Haiti n.k amekuwa akitamani sana kuja kuhubiri nchini Tanzania.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.