MTANGAZAJI

UIMBAJI UINGEREZA

Royal Advent Quartet wakiimba nchini Uingereza mwaka 2004


Miongoni mwa makundi ya waimbaji hapa Tanzania ambayo yamekuwa yakiwabariki na kuwapatia matumaini wasikilizaji wa AWR ni kundi la Royal Advent Quartet la mjini Morogoro linaloundwa na waimbaji wanne Mbaraka Mchome,Yona Msomi,Simon Mdee na mimi(Maduhu Jumanne).

Nikiwa na kundi hili tulibahatika kwa mara ya kwanza kualikwa na Kanisa la Angaza lililoko ,Reading, Berkshire nchini Uingereza ambako tulitoa huduma ya uimbaji katika mahubiri ya hadhara ambapo mhubiri alikuwa Mchungaji William Mtani.

Tukiwa nchini humo kwa muda usiopungua miezi mitatu tulitoa huduma ya uimbaji katika sehemu mbalimbali,siku ambayo sitaisahau nikiwa Uingereza ni tulipoimba kwenye mkutano uliwakutanisha mamia ya watu katika ukumbi wa kisasa wa Area 5 The Globe Church Centre,Reading Oktoba 16,2004

Si tu kutokana na wingi wa watu bali ni kutokana na kuona na kusikia vikundi na kwaya za aina mbalimbali za uimbaji vikiimba siku hiyo.


AMA KWA HAKIKA BWANA YU MWEMA

4 comments

Vimax Pills said...

thanks for sharing

Obat Vimax said...

nice blog and article

Vimax Canada said...

nice blog and article, thanks for sharing

Selaput Dara Buatan said...

thanks you for sharing

Mtazamo News . Powered by Blogger.