MTANGAZAJI

WAADVENTISTA MAREKANI KUJADILI KANISA, SERIKALI NA USHUHUDA KWA UMMA.

 


Divisheni ya Amerika Kaskazini ya Kanisa la Waadventista wa Sabato (NAD) itakuwa mwenyeji wa mkutano mwezi Oktoba mwaka huu utakaochunguza uelewa wa kihistoria wa Kanisa hilo kuhusu uhusiano kati ya kanisa na serikali, pamoja na utume wake kwa umma katikati ya ongezeko la mgawanyiko wa kisiasa na kuibuka kwa utaifa wa Kikristo nchini Marekani.

Mkutano huo, wenye mada huu inayohusu Masalio na Jamhuri: Utambulisho wa Kinabii, Ushuhuda kwa Umma, na Changamoto ya Utaifa wa Kikristo, utafanyika Oktoba 14–17 katika Chuo Kikuu Waadventista cha Union,Lincoln, Nebraska. Ukiandaliwa na Idara ya Kumbukumbu, Takwimu, na Utafiti ya Divisheni ya Amerika Kaskazini pamoja na Idara ya Masuala ya Umma na Uhuru wa Kidini , tukio hili litawaleta pamoja wasomi, wachungaji, walimu, wanafunzi, viongozi wa kanisa, na washiriki ili kuchunguza uhusiano wa kihistoria na wa sasa wa Waadventista na masuala ya kisiasa.

Mkutano huu unakuja wakati Marekani inaadhimisha miaka 250 tangu kuanzishwa kwake, na unalenga kujadili namna Waadventista wanavyopaswa kuonyesha uelewa wao wa unabii kuhusu uhusiano wa kanisa na serikali katikati ya mgawanyiko mkubwa wa kisiasa na ongezeko la siasa za kidini. 

Kupitia mada mbalimbali zinazohusu thiolojia, historia, na uchambuzi wa kijamii na kisiasa, waandaaji wanatumaini washiriki watapata uelewa mpana wa namna mwito wa kipekee wa Waadventista unavyoweza kufuatwa katika makanisa mahalia na katika jamii kwa ujumla.

Mkutano huo utajumuisha orodha pana ya waandishi wa habari, wanahistoria, wanathiolojia, wachungaji, na watetezi wa uhuru wa dini kutoka ndani ya Kanisa la Waadventista na kutoka taasisi mbalimbali za kitaaluma.

Wahudumu watakaohudhuria ni pamoja na mwandishi wa habari, mwandishi wa vitabu, na mchambuzi wa masuala ya dini na siasa nchini Marekani  Katherine Stewart, Mwanathiolojia Matthew D. Taylor, Mwanahistoria Randall Balmer, Mchungaji wa muda mrefu wa Waadventista Dwight K. Nelson, Mwanathiolojia Maury Damon Jackson, Mwandishi na mwanahistoria Warren Throckmorton, Mwanahistoria Elesha Coffman, Profesa wa dini kutoka Chuo Kikuu cha Loma Linda Jeffrey Rosario, Mwanahistoria wa kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Andrews Kevin M. Burton, Mwanahistoria wa Waadventista Douglas Morgan, Mkurugenzi wa Kumbukumbu, Takwimu, na Utafiti wa NAD Michael W. Campbell na msaidizi wa mkurugenzi wa Masuala ya Umma na Uhuru wa Kidini wa NAD Melissa Reid, na mhariri wa Liberty Magazine Bettina Krause.




No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.