SABABU ZA BAADHI YA WAMAREKANI KUISHI PAMOJA BILA NDOA
Kuishi pamoja bila kufunga ndoa inaonekana limekuwa jambo la kawaida miongoni mwa watu wazima nchini Marekani. Kwa mujibu wa utafiti wa muda mrefu wa Kitaifa wa Maendeleo ya Vijana 1997 (NLSY97) uaonesha kuwa , takribani asilimia 77 ya Wamarekani wenye umri wa miaka 38–43 wamewahi kuishi na mpenzi bila ndoa katika kipindi fulani cha maisha yao. Hali hii inaonyesha mabadiliko makubwa ya kijamii na mtazamo mpya kuhusu mahusiano, ndoa na maisha ya familia.
Utafiti wa (NLSY97) ni moja ya tafiti kubwa na za kipekee zilizowahi kufanywa nchini Marekani. Utafiti huu umefuatilia maisha ya kundi moja la vijana kwa zaidi ya miaka 25, ukichunguza safari yao kutoka utotoni hadi utu uzima.
Utafiti huo unaonyesha tofauti kubwa kutokana na kiwango cha elimu. Watu wenye elimu ya sekondari au chini yake wana uwezekano mkubwa zaidi (82%) wa kuishi na mpenzi bila ndoa, ikilinganishwa na wale wenye shahada ya chuo kikuu (70%). Pia, walio na shahada wana uwezekano mkubwa wa kuishi na mpenzi mmoja tu, huku wengine wakiripoti kuishi na zaidi ya mpenzi mmoja katika nyakati tofauti.
Tofauti za umri pia ni sababu. Takribani asilimia 27 ya watu waliowahi kuishi na mpenzi walianza kabla ya kufikisha miaka 20. Hata hivyo, idadi hii ni kubwa zaidi kwa wale wenye elimu ya chini (40%) na ndogo kwa wenye shahada ya chuo kikuu (12%). Wenye elimu ya juu mara nyingi huanza kuishi na wapenzi mwishoni mwa miaka 20 au miaka 30, wakionyesha mtazamo wa kuchelewesha hatua za mahusiano ya kujenga familia.
Takwimu nyingine za utafiti huo zinaonyesha kuwa theluthi mbili ya watu waliowahi kuishi na mpenzi bila ndoa hatimaye huolewa na mpenzi huyo. Kati ya hao, asilimia 70 huolewa na mpenzi wa kwanza waliyeishi naye. Hata hivyo, tofauti za elimu na asili zinaonekana wazi kuwa Wazungu wanaongoza kwa kuolewa na mpenzi waliyeishi naye (73%), wakifuatiwa na Wahispania (59%) na Weusi (46%).
Kwa wastani, mahusiano ya kuishi pamoja bila ndoa hudumu miezi 18 kabla ya kuishia kwenye ndoa au kuachana. Lakini baadhi hudumu kwa miaka mingi. Takribani asilimia 26 ya watu wenye umri wa miaka 38–43 wamewahi kuwa na uhusiano uliodumu angalau miaka 5, huku 8% wakiripoti mahusiano yaliyodumu miaka 10 au zaidi. Watu wenye elimu ya chini wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa na mahusiano ya muda mrefu ya kuishi pamoja.
Kuishi pamoja bila ndoa nchini Marekani ni sehemu ya mabadiliko ya kijamii yanayoendelea kuunda sura mpya ya mahusiano ya kimapenzi. Elimu, asili, na umri vinaathiri kwa kiasi kikubwa jinsi watu wanavyoingia na kuendeleza mahusiano haya. Ingawa si mahusiano yote yanayoishia kwenye ndoa.

.png)
Post a Comment