WAADVENTISTA WATOA TAARIFA YA KANISA LILILOUNGUA
Konferensi ya Kati ya California ya Waadventista wa Sabato nchini Marekani imetoa taarifa rasmi kufuatia moto wa Juni 29 mwaka huu uliounguza Kanisa la Kihistoria la San Francisco lililopo katika eneo la Lower Pacific Heights, jijini humo.
Kwa mujibu wa konferensi hiyo, moto ulizuka Jumatatu alasiri katika kanisa hilo lililoko kwenye kona ya mtaa ya California na Broderick. Zaidi ya wazimamoto 100 walijitokeza, hatua iliyosababisha amri ya watu kubaki nyumbani, kufungwa kwa barabara na kukatika kwa umeme katika maeneo ya jirani. Hadi jioni, wazima moto walikuwa wameudhibiti moto, lakini vikosi vilibaki eneo hilo usiku kucha kufuatilia hali ya jengo.
“Hakuna majeruhi waliyoripotiwa,” konferensi ilisema, ikiongeza kuwa kulinda waumini, majirani, wahudumu wa dharura na jamii inayozunguka eneo hilo ndiyo kipaumbele chao cha juu.
Jengo la kanisa hilo, lililojengwa mwaka 1892, limekuwepo katika eneo hilo kwa zaidi ya karne moja. Tangu waumini wa kiadventista walipolinunua mwaka 1927, limehudumia vizazi mbambali vya waumini na kuendesha huduma hai za kanisa jijini San Fransisco.
Wachunguzi bado hawajabaini chanzo cha moto. Hata hivyo, Mamlaka zinaeleza kanisa lilikuwa katika ukarabati wakati moto ulipoanza. Alisema wafanyakazi walikuwa eneo la tukio na shughuli za ujenzi huenda ndizo zilizosababisha moto huo. Idara ya Zimamoto ya San Francisco
Viongozi wa kanisa bado wanakadiria kiwango cha uharibifu, lakini pia wanahofia kuwa huenda vitu kadhaa vya kihistoria vilivyokuwa ndani ya jengo vimepotea. Miongoni mwa vitu hivyo ni mimbari ya karne iliyochongwa kwa mkono kwa kutumia mti wa walnut, ambayo ni sehemu muhimu ya historia ya Waadventista. Kwa mujibu wa rekodi za kanisa, waanzilishi akiwemo J. N. Loughborough, James White, Ellen G. White, D. M. Canright na viongozi wengine wa mwanzo wa kanisa waliwahi kuhubiri wakiwa kwenye mimbari hiyo lilipokuwa katika Kanisa la Laguna huko San Francisco. Viongozi hawajathibitisha kama mimbari hiyo ya kihistoria imeokoka na moto.
Katika taarifa yake, Konferensi iliwashukuru wazima moto kwa mwitikio wao wa haraka na kuonyesha shukrani kwa msaada uliotolewa na waumini na jamii ya eneo hilo.
Konferensi pia ilitangaza kuwa Kanisa la Philadephia la San Francisco litawapokea waumini wa kanisa lililoungua kuanzia Sabato ya Julai 4, baada ya kufungua milango yake kwa familia ya kanisa lililopoteza mahali pa ibada.

.png)
Post a Comment