MGHANA AKIRI ULAGHAI WA KIMAPENZI WA DOLA MILIONI 4.
Raia wa Ghana aliyekabidhiwa kwa serikali ya Marekani amekiri kuwa na hatia ya kula njama ya kutenda ulaghai wa mtandao (wire fraud) kuhusiana na ulaghai wa kimapenzi na urithi uliolenga kuwahadaa wazee na kujipatia dola milioni 4.4 za kimarekani.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Marekani wa Wilaya ya Arizona, Joseph Kwadwo Badu Boateng alikamatwa nchini Ghana Mei 27, 2025 kwa hati ya kukamatwa kwa ajili ya kukabidhiwa. Alikabidhiwa kwa Marekani mwezi Juni 2025 na amekuwa kizuizini tangu wakati huo.
Uchunguzi uliendeshwa na ofisi ya FBI Phoenix Division, tawi la Sierra Vista.
Msaada ulitolewa na ofisi ya FBI ya masuala ya kisheria mjini Accra, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Wizara ya Sheria ya Ghana, Ofisi ya Uhalifu wa Kiuchumi na Uhalifu Ulioandaliwa ya Ghana, Huduma ya Polisi wa kimataifa ya Ghana – INTERPOL, na Ofisi ya Masuala ya Kimataifa ya Wizara ya Sheria ya Marekani.
Katika makubaliano yake ya kukiri hatia, Boateng alikubali kwamba yeye na washirika wake waliendesha mpango wa ulaghai wa kimapenzi na urithi kati ya mwaka 2013 na Machi 2023, wakilenga wazee huko Arizona na maeneo mengine ya Marekani.
Washirika hao walijifanya kuwa wapenzi kupitia majukwaa ya kutafuta wenzi mtandaoni, ujumbe mfupi na mawasiliano mengine ya kielektroniki.
Pia walidai kwa uongo kuwa wamepokea “urithi” wa dhahabu na vito.
Katika taarifa, Idara ya Sheria ilisema walaghai hao waliwaambia waathiriwa kwamba kulikuwa na kodi na ada zilizohitajika ili kuachiwa mali hizo.
Taarifa hiyo ilisema: “Mbali na kukiri hatia, Boateng amekubali kulipa fidia ya takribani dola milioni 4.4, ambayo ndiyo hasara ya moja kwa moja iliyosababishwa na ushiriki wake katika mpango huo. Hukumu ya Boateng imepangwa kutolewa Septemba 8 2026, mbele ya Jaji wa Mahakama ya Wilaya nchini Marekani Angela M. Martinez.

.png)
Post a Comment