MTANGAZAJI

KIJANA TOKA TANZANIA AFARIKI BAADA YA KUZAMA MTONI NCHINI MAREKANIAllen Buberwa enzi za uhai wake (Picha na 5newsonline.com)

Mamlaka ya Serikali ya Kaskazini Magharibi mwa Jimbo la Arkansas nchini Marekani zinaeleza kuwa Mwanafunzi katika Chuo cha Arkansas Allen Buberwa (22)  toka Tanzania amefariki dunia baada ya kuzama katika Mto Buffalo.

Buberwa aliingia Marekani Disemba mwaka jana na akajiunga katika chuo hicho kilichopo karibu na Mji wa Harrison akiwa miongoni mwa wanafunzi wanaotoka mataifa mbalimbali nje ya nchi hiyo.

Afisa wa Polisi katika Mji wa Newton  Glenn Wheeler  katika taarifa yake ya Mei 7 ambayo pia imewekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Jeshi la Polisi la mji huo ameeleza kuwa Buberwa alifariki jumatatu ya Mei 6 mwaka huu baada ya kuzama katika eneo la mto huo liitwalo  Pruitt Landing kilomita 169 toka Kaskazini Magharibi mwa jiji la Little Rock.

Wheeler  amesema mashuhuda walimwona  Buberwa  akiteleza na kuzama ndani ya mto ambapo mtu mmoja alijitosa kumwokoa lakini naye akataka kuzama ambako waokoaji walimwokoa mtu huyo lakini Marehemu hakuonekana.

Taarifa ya Afisa huyo wa Polisi imeeleza kuwa mwili wa Buberwa  ulipatikana saa tano baada ya kuzama.No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.