JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO DALLAS TEXAS, MAREKANI YAPATA UONGOZI MPYA
Katibu Mkuu Godfrey Mwamsoyo |
Everest Michael, Mwenyekiti mpya. |
Jumuia ya Watanzania waishio katika jiji la Dallas,Texas Marekani
Tanzanians Dallas,Januari 12 mwaka huu imefanya mabadiliko ya uongozi kwa kuwachagua viongozi mpito watatu.
Uchaguzi huo ulihudhuliwa watanzania waishio katika eneo hilo na kufanya maamuzi ya uongozi wa
dharura kutokana na kujiudhuru kwa uongozi uliyopita.
Watanzania
katika jiji hilo la Dallas na vitongoji vyake wanaamini kwamba,
mshikamano wao ambao ndio kilikuwa ni chanzo kikubwa cha wao kuwa kitu
kimoja wakati wa misiba
na dharura za aina yote kimaisha wanavyoishi ughabuni. Kufuatana
na katiba ya jumuiya hiyo kikao kiliteua wagombea wa mpito mpaka hapo mwezi Julai katika uchaguzi
mkuu chini ya utaratibu mpya.
Uongozi
uliotumikia jumuiya hiyo kwa muda sasa na hatimae kujiudhuru kwa
hiyari, ni mwenyekiti Bw. Benedict Kazora, Bi Maria Musomi, Makamo
mwenyetkiti na Katibu Bi Viola Mbise.
Maamuzi hayo ambayo yanaelezwa kuwa yalikuwa ya ghafla yaliwakilishwa kwenye kamati ya ushauri
na kutangazwa rasmi katika tofuti za mitandao ya kijamii mara moja.
Harakati zipo mbioni kuwasiliana na uongozi uliopita kukabidhiana
nyaraka na uongozi mpya mpito haraka iwezekanovyo.
Jumuiya
hiyo, imewachagua viongozi wake mpito wapya kupitia utaratibu wa
kuwapigia kura wale wote walioteuliwa na wanajumuiya baada ya mkutano
huo mahususi kuziba hizo
nafasi hizo.
Waliochaguliwa ni Mwenyekiti ni
Bw. Everest M. Michael, Katibu Bw. Godfrey Mwamsoyo na mweka hazina ni
Bi Jocyline Vadesto.
Post a Comment