KONGAMANO LA TAUS KUFANYIKA SAN DIEGO CALIFORNIA MAREKANI JULAI 11-15,2018
Baadhi ya wanachama wa TAUS waiohudhuria kongamano la mwaka 2017 huko Wisconsin |
Kongamano la Umoja wa Waadventista waishio nchini Marekani (TAUS) linatarajiwa kufanyika huko San Diego California katika hoteli ya Pala Mesa kuanzia Julai 11 hadi Julai 15 mwaka huu ambapo mnenaji mkuu atakuwa ni Mchungaji Baraka Butoke Jr toka Tanzania
Mwenyekiti wa TAUS Michael Mwasumbi ameuambia mtandao huu kuwa jumla ya wanachama 150 wamejiandikisha kushiriki tamasha hilo lenye kauli mbiu ya Mimi ni nani gundua utambulisho wako ambalo linalengo la kuwakutanisha wanachama wa TAUS kwa ajili ya uamsho wa kiroho,kufahamiana na kuweka mikakati mbalimbali ya kuendeleza miradi kadhaa nchini Tanzania inayoratibiwa na kufadhiliwa na umoja huo.
TAUS iliyoanzishwa mwaka 1999 na wanachama 25 huko Massachusetts nchini Marekani ikiwa na wanachama wapatao 300 inalengo la kufanya uinjilisti,na kufadhili masuala ya elimu na sekta ya afya hasa nchini Tanzania ambako wanachama wake wanatoka.
Miongoni mwa miradi inayoendelea kusimamiwa na TAUS nchini ni kusomesha na kufadhili wainjilisti na wainjilisti wa kiadventista,ujenzi wa makanisa,uboreshaji wa kituo cha Afya cha Kanisa la Waadventista Wa Sabato kilichopo kusini mwa Tanzania na kufadhili baadhi ya vifaa vya Morning Star Radio.
Post a Comment