MTANGAZAJI

ITAZAME VIDEO MPYA YA KUTIMIZA MIAKA 45 YA HERITAGE SINGERS


 


Hatimaye Santuri Mwonekano ya Kutimiza miaka 45 ya Waimbaji wa Heritage imeshatoka,Santuri hiyo ilirekodiwa Julai 30,2016 ikiwahusisha waimbaji zaidi ya 100 waliowahi kuimba na wanaimba mpaka sasa ambapo tiketi katika tamasha hilo lililofanyika huko Ontario,California  ziliuzwa kwa bei ya dola za kimarekani 25, 40, 55 na 95.

Hivi karibuni kupitia ukurasa wa Facebook wa Heritage Singers waimbaji hao wamekuwa wakiweka video fupi fupi za kuitangaza santuri hiyo na sasa tayali wameweka wimbo mmoja wa dakika 4:09 ulioko kwenye santuri hiyo ya masaa matatu kwenye wasifu wao wa  mtandao wa Youtube na mpaka leo Disemba 3 saa 9:00 alasiri tayali imeshatazamwa mara 1,328 .

Heritage Singers walianza kuimba mwaka 1971 huko Portland, Oregon, nchini Marekani na wamekuwa wakifanya matamasha ya uimbaji katika sehemu mbalimbali duniani ambapo wamefika katika majimbo 50 ya Marekani na nchi zaidi ya 75 miongoni mwa nyimbo zinazotarajiwa kuwepo katika santuri hiyo ni  “Jesus is the Lighthouse,” “Peacespeaker,” na "What a Day That Will

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.