DAR ES SALAAM:TANESCO YATANGAZA KUKATIKA KWA UMEME JUMA NZIMA NCHINI
Shirika la umeme
nchini (Tanesco), limetangaza nchi kuingia ‘gizani’ kwa juma zima kuanzia leo Septemba 7,2015
kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi inayozalisha umeme kutoka Songosongo na
kuanza majaribio ya gesi ya Mtwara inayosafirishwa kuja Kinyerezi jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu
wa Tanesco, Felchism Mramba, amewaambia waandishi wa habari hivi karibuni kuwa
baada ya kutembelea mtambo wa Kinyerezi I, sasa Watanzania wategemee umeme wa
uhakika baada ya kuanza kuzalisha umeme kwa gesi ya Mtwara.
Kwa mujibu wa
Mramba, mikoa itakayoathirika ni yote inayopata umeme wa gridi ya Taifa ukiwamo
Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Morogoro, Singida,
Mwanza, Mara, Mbeya, Iringa, Tabora, Shinyanga, Manyara na Zanzibar.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Dk. James Materegeo, amesema
mchakato wa kuchukua gesi kutoka mitambo ya Madimba mkoani Mtwara imekamilika
juzi na kazi inayofanyika ni ya majaribio.
Amesema
uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi ya Mtwara utaisaidia serikali kuokoa
takribani Dola za Marekani bilioni moja kwa mwaka ambazo zilikuwa zinatumiwa
kununua mafuta mazito ya kuzalisha umeme.
Post a Comment