MTANGAZAJI

VIDEO:MAHOJIANO NA MHE.ALHAJI ALI HASSAN MWINYI KUHUSU KISWAHILI


Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi zaidi kusini mwa jangwa la Sahara. 

Ni lugha ya taifa kwa nchi za Kenya na Tanzania na pia yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda, Visiwa vya Comoro na nchi nyingine,Ikizungumzwa na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika. 

Ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na hata usalama miongoni mwa mataifa. Lakini , licha ya ukubwa wake, lugha hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Hivi karibuni, Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kilifanya mkutano wake wa nne, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi. Na amekuwa mkarimu sana kujiunga nasi kuzungumzia juu ya lugha ya Kiswahili na changamoto zake.
KARIBU

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.