MTANGAZAJI

RAIS KIKWETE ATAKA KUUNDWA KAMATI YA KUSHUGHURIKIA KUTEKWA NA KUUAWA KWA WALEMAVU WA NGOZI (ALBINO)

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete ameamrisha kuundwa kwa kamati maalum kutoka katika upande wa serikali, watu wenye ualbino pamoja na jukwaa la tiba asilia haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha kamati hiyo itashughulikia ipasavyo matukio ya utekaji nyara na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanayoendelea nchini Tanzania. 

Hapo jana Rais kikwete alishindwa kuonana na ujumbe wa watu kumi na nane kwa wakati maalum uliopangwa kutokana na baadhi ya watu wenye ualbino kuanzisha vurugu ukikataa ujumbe huo kwa madai kuwa muda wa kukaa madarakani kwa viongozi wa chama cha watu wenye ualbino TAS umekwisha muda wake.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.