RAIS KIKWETE AANZISHA UJENZI WA DARAJA KILOMBERO
Historia
imeandikwa jioni ya jana, Jumatano, Agosti 20, 2014 katika Mkoa wa
Morogoro na katika Tanzania. Kwa mara ya kwanza tokea enzi na enzi,
magari yameweza kuvuka Mto wa Kilombero, moja ya mito mikubwa zaidi
nchini, mpakani mwa Wilaya za Ulanga na Kilombero katika Mkoa wa
Morogoro.
Magari
hayo ya msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete yamevuka Mto Kilombero kwa kutumia daraja dogo la
muda ambalo wajenzi wa daraja kwenye mto huo wamelijenga kwa ajili ya
kurahisisha kazi yao ya ujenzi wa daraja hilo kubwa. Daraja hilo la muda
la chuma lina uwezo wa kubeba tani 100.
Rais
Kikwete na msafara wake wa magari kiasi ya 20 umevuka Mto Kilombero kwa
kutumia magari ukitokea Wilaya ya Ulanga kuingia katika Wilaya ya
Kilombero kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja hilo
katika sherehe iliyofanyika upande wa mto wa Wilaya ya Kilombero,
kilomita kiasi cha saba unusu kutoka mjini Ifakara.
Rais
Kikwete ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Daraja la Mto Kilombero
kwenye siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku saba katika Mkoa wa
Morogoro.
Rais
Kikwete ameanzia ziara hiyo katika Kijiji cha Mwaya ambako amezindua
Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini na pia kuzindua Mradi wa Mfumo wa
Huduma za Afya za Masafa (Telemedicine).
Daraja
hilo linalojengwa kwenye Mto Kilombero unakamilisha ujenzi wa madaraja
matano makubwa nchini ambayo yalikuwa yamepangwa kujengwa katika Mpango
wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo mwaka wa fedha wa 1967-1968 lakini
likashindikana kujengwa kwa miaka 47 iliyopita mpaka sasa.
Daraja
hilo linalogharimu Sh. bilioni 55.8 ambazo zote zinatolewa na Serikali
ya Tanzania linajengwa na Kampuni ya China Railway 15 ya China, lina
madaraja mawili – kubwa ambalo lina urefu wa mita 384 na dogo lenye
urefu wa mita 120, litakuwa pia na makaravati 35, na njia ya watu kupita
kwa mguu na baiskeli.
Daraja
hilo lenye uwezo wa kubeba tani 180 kwa wakati mmoja, pia litajengwa
pamoja na barabara ya lami ya kilomita 9.5, ikiwa ni kilomita saba unusu
upande wa Ifakara na kilomita mbili upande wa Wilaya ya Ulanga.
Akizungumza
kwenye sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi
pamoja na kwamba Rais Kikwete alikawia kidogo kufika darajani hapo kwa
sababu ya shughuli za uzinduzi wa miradi mingi kwenye Wilaya ya Ulanga,
Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Mhandisi Patrick Mufugale amesema kuwa ujenzi
wa daraja hilo umechelewa kidogo kwa sababu ya tuta na daraja la mwanzo
la muda kuchukuliwa na maji wakati wa mafuriko ya mwaka huu.
Amesema kuwa kutokana na tukio hilo, ujenzi wa sasa umefanyiwa marekebisho makubwa ambayo yataliwezesha tuta la sasa kuweza kuhimili aina yoyote ya mafuriko makubwa hata kwa miaka 100 ijayo.
Amesema kuwa kutokana na tukio hilo, ujenzi wa sasa umefanyiwa marekebisho makubwa ambayo yataliwezesha tuta la sasa kuweza kuhimili aina yoyote ya mafuriko makubwa hata kwa miaka 100 ijayo.
Baada ya kushindikana kujengwa kwa miaka mingi, Rais Kikwete, wakati akiwa Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 aliahidi ujenzi wa daraja hilo. Aidha, ujenzi huo uliwekwa katika Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Akizungumza
na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja hilo na
kupanda Mti wa Kumbukumbu, Rais alikumbusha historia ya ujenzi wa daraja
hilo akisema kuwa katika Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo,
Serikali iliamua kujenga madaraja matano makubwa nchini.
Amesema
kuwa madaraja hayo ni Daraja la Kirumi kwenye Mto Mara, Daraja la Mto
Rufiji, Daraja la Kigamboni, Dar Es Salaam; Daraja la Mto Kilombero na
Daraja la Mto Malagarasi.
Amesema
kuwa kati ya madaraja hayo, Uongozi wa Awamu ya Kwanza ulijenga Daraja
la Kirumi kwenye Mto Mara na Uongozi wa Awamu ya Tatu ukajenga darala la
Mto Rufiji.
“Sisi
tuliamua kujenga madaraja matatu makubwa – Kigamboni na kwenye Mito
Malagarasi na Kilombero. Lile la Malagarasi limekamilika, lile la
Kigamboni linakamilika na litakuwa tayari Juni, mwakani, wakati leo
tumeweka jiwe la msingi kwenye Ujenzi wa hili la Kilombero ambalo ujenzi
wake tayari umeanza.”
Rais Kikwete ambaye ameanza ziara ya Mkoa wa Morogoro jana, leo aliendelea na ziara yake katika Wilaya za Morogoro
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
20 Agosti,2014
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
20 Agosti,2014
Post a Comment