WANANCHI WA KILOSA WAMLALAMIKIA MKURUGENZI WA HALMASHAURI
Wananchi
katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamelalamikia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu Masalu Mayaya kwa madai ya kutotekeleza wajibu wake katika kusimamia
maendeleo ya sekta ya Afya.
Wananchi hao
wametoa malalamiko hayo kufuatia kuwapo
kwa madai kuwa hospitali ya wilaya ya hiyo imetelekezwa na hivyo kukosekana kwa huduma
muhimu vikiwemo vifa tiba na dawa.
Wananchi hao
wamesema kuwa kukosekana kwa huduma bora za afya katika hospitali hiyo ya wilaya
kumesababishwa na mkururgenzi
huyo kutokemea matumizi mabaya ya
fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya umma.
Kwa upande
wake mkurugenzi huyo amesema tayari
ofisi yake imeanza kufuatilia maagizo ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Ameir Mbaraka kuhusu fedha za miradi ya jamii
zilizotengwa mwaka jana.
Amesema
haoni sababu za yeye kulaumiwa na kupigiwa kelele kama aliyefanya uhalifu badala yake wananchi wanapaswa
kuzingatia ukweli kuwa huduma za afya katika hospitali ya wilaya ni
changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi na kuwa hakuna matatizo makubwa.
Mayaya
ameongeza kusema kuwa jamii inapaswa
kutambua majukumu yake ya halmashauri
pamoja na kuacha tabia ya kuwaingiza watendaji katika tuhuma za
ubadhilifu na ufisadi ,badala yake wawe
na subira kuona jinsi wanavyoshughulikia
matatizo yanayokabili sekta hiyo.
Post a Comment