WAOSHA KUCHA NA MIGUU WANAVYOINGIZWA KATIKA HATARI YA KUAMBUKIZWA VVU
Utengenezaji wa kucha na uoshaji miguu ni biashara
inayokuwa kwa kasi hasa maeneo ya mijini ambapo wanawake wengi wanahusudu na
kujihusisha na masuala ya urembo.
Uchunguzi unaonyesha kuwa wakati wa ufanyaji wa shughuli hiyo, hutokea baadhi ya wanawake wakaoshwa au kusuguliwa sehemu za miguu zinazokaribia maeneo ya mapaja, hivyo kuamsha hisia kati ya mtoa huduma na mpokea huduma.
Hatua hiyo inatajwa kuwasababashia baadhi yao
kufanya ngono ambayo mara nyingi siyo salama, wanapotoa huduma katika maeneo
tulivu ikiwamo saluni maalumu na nyumbani kwa wateja.
Mmoja
wa wafanyabiashara hiyo katika Soko la Mwenge Hamis Shaban(19) (siyo jina
halisi) anasema kuwa kuna wakati wamekuwa wakiingizwa katika mtego na wateja.
Yule sista
amenifanyia vituko muda mrefu, nikaona asije kunitangazia vibaya bure kwamba
mimi siyo mwanaume kamili; hivyo kumwonyesha kuwa nimekamilika, nikalazimika
kufanya, ingawa sasa hivi unavyoniuliza naanza kupata wasiwasi.
Anasema kuwa hali hiyo hutokea mara nyingi hasa mteja
anapotaka kwenda kuhudumiwa nyumbani kwake, ambapo hukuta tayari wameandaa
mazingira, ambayo mwisho wake huishia katika hatua hiyo.
“Mimi mwenyewe imenitokea siku chache zilizopita;
kuna binti fulani amekuwa mteja wangu kwa muda mrefu, amekuwa akinifanyia
vituko vya hapa na pale. Nilikuwa sijali, ila majuzi akaniambia niende kwake
nikamchore tattoo,”anasema Shaban na kuongeza:
“Eneo alilotaka nimchore ndilo lilianza kunipa
wasiwasi, lakini kwa sababu ya pesa nikapiga moyo konde. Akavua blauzi yake na
kutaka nimchore kwenye titi; nilijaribu kutimiza wajibu wangu, lakini mambo
ambayo alikuwa akifanya, yalinisababishia uzalendo kunishinda, hatimaye
tukajikuta tukifanya ngono.”
Anafafanua kuwa sababu nyingine iliyosababisha
kufanya ngono ilikuwa kutaka kujenga heshima kwa mteja wake huyo, ili amwone
kuwa ni mwanaume aliyekamilika.
“Yule sista amenifanyia vituko muda mrefu, nikaona
asije kunitangazia vibaya bure kwamba mimi siyo mwanaume kamili; hivyo
kumwonyesha kuwa nimekamilika, nikalazimika kufanya, ingawa sasa hivi
unavyoniuliza naanza kupata wasiwasi.”
Mahamod Abdalah anayefanya biashara hiyo eneo la
Makumbusho, naye anakiri kuwepo na changamoto mbalimbali, ambazo huwafanya
wengi wao kuingia kwenye mitego na kufanya kazi ya kuwafurahisha wake za watu.
“Hiyo changamoto kweli ipo, inahitaji moyo wa ziada
kukabiliana nayo. Wanakuja wanawake wa haja, utakuta anakufunilia maungo,
anataka umsugue; yaani hatari tupu, sasa kama huna ujasiri, lazima utaingia
kwenye mtego.”
Chanzo:Gazeti la Mwananchi
Post a Comment