MTANGAZAJI

RAIS KIKWETE AKERWA NA UANDISHI WA VICHWA VYA HABARI KUHUSU EAC

Picture
Jambo Leo
Picture
Tanzania Daima
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amevitaka vyombo vya habari vya Tanzania kuonesha ukomavu katika kuisaidia nchi kujenga mahusiano na nchi nyingine badala ya kuandika na kutangaza habari za uhudisiano kwa ushabiki na utiaji chumvi.

Wito huo wa Rais Kikwete unafuatia uandishi wa habari za mkutano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mheshimiwa Bernard Membe na Waziri wa Mambo ya N\!je wa Kenya, Mheshimiwa $Aina Mohammed uliofanyika jana, Jumapili, Novemba 10, mjini Dar es Salaam.
Kufuatia hatua hiyo muhimu na sahihi ya Kenya, baadhi ya magazeti yaliyochapishwa novemba 11 mwaka huu nchini Tanzania yametoka na vichwa vya habari , “Kenya yaiangukia Tanzania” na “Kenya wasalimu amri”, vichwa vya habari ambavyo havisemi ukweli, siyo sahihi na ni vya uchochezi na uzandiki.

Vichwa vya habari ambavyo haviitendei haki Tanzania wala Kenya. Rais Kikwete hakufurahishwa, na kwa hakika, amesikitishwa na vichwa hivyo vya habari.

Tanzania, kupitia hotuba ya 
Rais Kikwete Bungeni Alhamisi iliyopita ilitoa hoja za kuimarisha Jumuia ya Afrika Mashariki. Kenya imeelewa hoja hiyo ya Tanzania na imefanya uamuzi sahihi na wenye manufaa kwa Jumuia yetu.

Hivyo, ni wajibu wa vyombo vya habari nchini kuchangiakatika kuimarisha 
Jumuia badala ya kuandika habari zautengamano kwa namna ya ushabiki usiokuwa na maana nausio na mashiko.

Imetolewa na

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
Dar es  Salaam.
Novemba 11,2013

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.