MTANGAZAJI

MAONI YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA TANZANIA MHE BERNARD MEMBE KUHUSU SAKATA LA MELI ZA IRAN


Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe

Mheshimiwa Bernard Membe kupitia ukurasa wake kwenye mtandao jamii wa facebook anasema  Serikali ya Tanzania imepokea taarifa kuhusu tuhuma za meli za Iran kupeperusha bendera za Tanzania ili kukwepa vikwazo. Serikali ya Jamhuri ya Muungano na SMZ hazitaki kupuuza taarifa hizi. Serikali zote mbili zimeamua kufanya uchunguzi ili kuthibitisha. 

Tanzania imewaarifu nchi zilizolalamika marafiki kuwaomba kusaidiana nasi kufanya uchunguzi na kushirikiana kuthibitisha taarifa hii. Tumefanya hivyo kwa kuzingatia uwezo wetu wa kiutafiti na kutaka utafiti huu kuwa huru kwa kuwashirikisha wao wenye ujuzi mkubwa. 

Tunafanya hivyo kwa kuwa wakala wa ZMA anayefanya kazi za kusajili amekana kusajili meli za Iran, Balozi wa Iran nchini aliitwa akakanusha. Tutakapopata matokeo ya utafiti na ikithibitika kuwepo na ukweli hatua zitachukuliwa mara moja. 

Tukithibitisha tuhuma hizi tutafutilia mbali usajili wa meli hizo. Tunafanya hivyo kutimiza wajibu wetu kimataifa hususan Azimio 1920 la UN Security Council.Tanzani sio adui wa nchi yoyote duniani. 

Tunafurahia mahusiano yetu na nchi zote duniani. Hili ni jambo linalogusa maslahi ya Tanzania nje na maslahi ya Tanzania ya ndani (Muungano), tujihadhari na namna tunavyolizungumzia. Tusimame pamoja kama taifa. Nchi kwanza!

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.