MTANGAZAJI

BARUA YA WAZI KWA WATANZANIA


Kanuni moja ya TANU ilikuwa inasema hivi: “Nitasema ukweli daima. Fitina kwangu ni mwiko.” Hii kanuni bado ni muhimu katika Tanzania ya leo. Leo ningependa kuongea na watanzania wenzangu wote, shangazi kule Mofu, mama tatu pale bagamoyo, na watanzania wote pale mlipo. Kila mmoja wetu anahitajika ili tuinusuru, tuikwamue na kuiendeleza nchi yetu. Baadhi ya watu watasema ninayo yaongea ni “uchochezi” waache wasema., “Nitasema ukweli daima. Fitina kwangu ni mwiko
Uongozi katika ngazi yoyote ile, na hasa zaidi katika ngazi zote za serikali ni dhamana tuliyowapa viongozi kuwakilisha na kutatua matatizo yetu. 

Leo viongozi wetu wanagombana kuhusu posho, wakati mwakilishi wetu wa serikali bungeni akitofautiana na msimamo alioutoa rais na wa serikali. Swali langu sasa ni upi msimamao wa serikali. Rais tunakuomba utoe tamko mbele ya watanzani wote kupitia kwenye TV msimamo wako na wa serikali. Tumekupa dhamana ya kutuongoza watanzania na serikali yako. Wakati mihimili mikuu ya serikali ikitofautiana kuhusu posho za wabunge (waziri mkuu ni mwakilishi was serikali bungeni, cha ajabu anatofautiana na msimamo wa rais). Kuna watu wanakufa kila siku kutokana na mgomo wa madaktari nao wakidai posho zao, lakini wabunge wetu na viongozi wetu wanasema kwamba wabunge ndiyo wanaostahili posho kutokana na majukumu yao, kwani baadhi ya posho zao wanatumia posho zao kuwapa mfano shangazi yangu pale mofu anayekula mlo mmoja kwa siku , au mama tatu pale bagamoyo mtoto wake anaumwa taabani. 

Swali kwa watanzania wenzangu je wewe umepata msaada gani kutoka kwa mbunge wako, wakati wewe unapata mlo mmoja kwa siku, au unahangaika kumtibu mwanao anayeumwa taabani, au unaposhindwa kununua mafuta ya taa kwa ajili ya matumizi yako?

Nitaongelea mambo makuu machache.  Kwanza Tanzania ni nchi yenye kila sababu ya kuwa mbali kimaendeleo Afrika tofauti na nchi nyingine. Tuna amani, tuna maliasili nyingi ambazo zinaweza kutukwamua.  Usiende mbali angalia jirani zetu wa Rwanda chini ya uoangozi wa rais Kagame wameanza kutuacha nyuma kimaendeleo, Tanzania ni nchi ya tatu duniani kupata misaada ya kimataifa kufuatia Iraq na Afghanistani, hii missada imekunufaishaje wewe uliye kijijini? Hi missada tunayopewa inakwenda wapi? Tunawataka viongozi wetu wote waweke wazi mikataba na misaada yote ili wananchi wote tuijue. 

“Nitasema ukweli Daima, fitina kwangu mwiko” Uongozi ni dhamana ya uaminifu wa wananchi kwa viongozi wao, nawapongeza viongozi wa kweli na wawazi, nawapongeza viongozi wachache, najua wapo wengi , lakini nakupongeza mheshimiwa Mwakembe, nakupa pole, mheshimiwa Sitta, vijana machacahari, Zito kabwe, January Makamba, David Kafulila, Mheshimiwa Slaa, Waziri wakuu wastaafu mzee Warioba, Mzee Sumaye, Dr Salim Ahmed Salim, na viongozi wengi wa vyama vya upinzani, na wengine ambao sijawataja. Nawapongeza kwa juhudi zenu za kutetea maslahi ya taifa na kuongea ukweli najua kazi ni ngumu na ni ya hatari.

Nawaomba watanzania wenzangu tuwalinde kwa hali na mali viongozi wanaotetea maslahi ya taifa, na kuwaeleza ukweli bila kuwaficha wale wanaotumia maslahi ya taifa kwa ajili yao na familia zao. Kumbuka si ajabu hata mbunge wako anayedai kwamba anatumia posho zake kuwasaidia wananchi wake, hata hajui na hajali kama jana ulilala na njaa, au ulilala mapokezi hospitalini kusubiri daktari wa kukutibu au kumtibu mtoto wako.

Serikali yetu inapoteza mwelekeo wa kutatua matatizo ya watanzania, kwa wengi wanatambua kwamba bei ya uzalishaji mafuta ya taa ni ndogo kuliko ya kuzalisha petrol, sasa inakuwaje bei ya mafuta ya taa ni ghali kuliko ya petroli? Mama Mwajuma hivi unatumia mafuta ya taa au petrol kupikia wanao chakula cha mlo mmoja wa siku, au kwenye kibatari chako? Serikali imeshinda kuwadhibiti wachakachuaji na kuamua kuongeza hela ya mafuta ya taa kwa ajili ya kupunguza tabia hii. Lakini serikali yetu hiyo hiyo, inafanya kila juhudi kuwadhibiti wale wanaodai haki zao za kimsingi na kikatiba, tutafika kweli? Wameongeza bei ya umeme, sasa mwenzangu Swai anaye choma grill pale ubungo ataweza kuhimili? Wakati mheshimiwa Rais alituahidi kutatua matatizo ya umeme katika term yake ya kwanza, lakini hadi leo kukosa umeme ni suala la kawaida na lililozoeleka. Misaada tunapewa ya kusaidia kutatua matatizo ya umeme lakini hatuyaoni, Wengine wanaingina mikataba isyo na tija kwa nchi, na kujitajirisha wao lakini kila leo tunawaona wanavojiona miungu watu. Watanzania “tuseme ukweli daima, ufitina uwe mwiko”

Watanzania tuache uoga wa kusema ukweli, Viongozi tuliowa chagua hatukuwachagua wawe miungu watu (wengine wameshazoea hilo),  Ni kweli watanzania ni waaminifu (watanzania wa kawaida), wakati wa uchaguzi unakuta wabunge wetu wanakuja kwa vizawadi vya kila aina ili tuwachague, halafu tunachukuli hii zawadi ni kama kiapo tulichokula, kwamba tutamchagua ingawa haangalii maslahi yetu. Nawaomba mjaribu hili, akikupa kanga, gunia la chele (wapogoro wenzangu) wakati akiomba kura, kuchukua na mwambie unawajua wengine pia ili na wao wapate. Siku ya uchaguzi tumia busara yako na haki yako ya kikatiba kumchagua yule unayemwona ni mwaminifu na anyejali maslahi ya taifa. Kwani aliyekupa kanga ua gunia la mchele hayuko nawe wakati ukipiga kura yako.
Watanzania tuanze kusema ukweli daima tuache ufitina.

Arthur Soni
Arthusoni2010@gmail.com

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.