MTANGAZAJI

ALIYEWAHI KUWA MTANGAZAJI WA MORNING STAR RADIO KUGOMBEA UBUNGE MOROGORO MJINI

Aliyewahi kuwa mtangazaji wa kipindi cha LULU ZA INJILI hapa Morning Star Radio 105.3 FM Amani Mwaipaja ametangazwa na CHAMA cha CHADEMA wilaya ya Morogoro mjini kuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwishoni mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa nabari ofisi kwake Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Morogoro mjini Zuber Tumaini alisema kuwa wao kama chama walikaa vikao mbalimbali vya kumjadilia mgombea huyo na kumteua kuwania nafasi kwa kuwa waliona ana sifa zinazofaa

Tumaini alisema kuwa mjumbe waliomteaua ni kijana ambaye ana stashahada ya sheria kutoka chuo kikuu Mzumbe hivyo ana uwezo mkubwa katika mambo ya sheria na ujasilamali kwa hiyo wananchi wategemee kupata tumaini jipya kiutawala na kisiasa
Kwa upande wake Amani Mwaipaja alisema kuwa kilichomsukuma kuitikia wito wa kugombea ubunge jimbo la Morogoro mjini kwamba jamii imekubwa na kero mbalimbali ila zikiwemo afya,barabara,maji na wanapata hela za kuendeshea miradi hiyo ila haifiki kwa wakati kwa kuwa hamna mtu wa kuwasemea katika seriakali

Mwaipaja alisema kuwa jamii itambue kuwa kupata uongozi sio mahali pakupumzika hivyo ni lazima wananchi wamchague mtu ambaye anakabilaiana na changamoto zao na kuzifanyia kazi kwa wakati mufaka bila kusubiri muda wake unapokaribia kuisha ndipo anaanza kuwa karibu na wananchi kwa lengo kuomba kurudi madarakani tena

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.