MTANGAZAJI

MVIWATA MMEWAONA HAWA???


Wakulima wakiuza matunda yao huko Dumila Morogoro

Viongozi wa Halmashauri za wilaya nchini, wameshauriwa kusaidia na kusimamia uendelevu wa masoko ya wakulima yanayojengwa vijijini na wahisani badala ya kuweka vikwazo vinavyoashiria kuua masoko hayo.

Wito huo umetolewa na wadau wa masoko sita ya wakulima yaliyojengwa na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), walipokutana juzi kwenye kikao cha pamoja kwenye soko la Kinole wilaya ya Morogoro.
Baadhi ya viongozi wa masoko walilalamikia vitendo vya halmashauri za wilaya kudai kodi kubwa kutoka kwenye masoko, huku halmashauri hizo zikiwa zimeshindwa kudhibiti masoko yasiyo rasmi yaliyoko jirani na zikishindwa kumaliza ubovu wa barabara unaokwamisha wafanyabiashara kupeleka magari kwenye masoko hayo.
MVIWATA kwa kushirikiana na wahisani mbalimbali imefanikiwa kujenga masoko sita ya wakulima vijijini. Masoko hayo ni pamoja na soko la Kimataifa la Nafaka la Kibaigwa Kongwa Dodoma, soko la matunda lililoko kijiji cha Kinole na soko la matunda na viungo la kijiji cha Tawa wilayani Morogoro.

Mengine ni soko la Mbogamboga la Nyandira wilaya ya Mvomero, soko la viazi na mahindi la Igagala wilaya ya Njombe na soko la matunda na nafaka na mazao mengine la Mkata wilayani Handeni Tanga.

Kujengwa kwa masoko hayo kumesaidia kuondoa tatizo la wakulima kunyonywa kwani masoko yote yanatumia mizani halali na badala ya vipimo vilivyokuwa vikitumika kukadiria uzito ni kama vile gunia la lumbesa na debe, ndoo na vingine vidogo kama vile kopo, bakuli na sado

MVIWATA iliyoanzishwa mwaka 1993 imefanikiwa kuwaunganisha wakulima kuwa na sauti moja na kuwa na jukwaa la kuzungumzia kutokana na kuanzishwa kwa mitandao katika ngazi za kimkoa, kiwilaya, kata na vijiji katika maeneo mbalimbali nchini.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.