MALIPO MBAGALA WIZI MTUPU
Mmoja wa wazee Mussa Mgeni wa Mbagala akionyesha hundi yake yenye thamani ya shilingi 168,000 alizolipwa kama fidia kutokana na nyumba yake kuathilika na mabomu hata hivyo mzee huyo asiyeweza kutembea ana umri wa miaka 76 alilia sana kutokana na kuwa nyumba yake ilikuwa ya gharama zaidi ya hiyo pesa aliyopewa(picha toka www.pwaniraha.com)
Wahanga wa mlipuko wa mabomu uliotokea April 29 mwaka huu huko Mbagala jijini Dar walianza kulipwa jana, japo malipo hayo yanaonesha kuwa mtu aliyekuwa amelipwa fidia kubwa ni aliyepata shilingi milioni 11 na aliyepata kiasi kidogo ni yule alipwa sh 30,000 jambo ambalo limeleta malalamiko makubwa kwa waathirika hao.
Zaidi ya wakazi 300 wa mtaa wa Mbagala kuu walijitokeza kwenye ofisi za halmashauri ya Manispaa ya Temeke jana kuchukua malipo ya fidia
Kilichonishangaza ni kusikia baadhi ya watangazaji wa kituo kimoja cha televisheni hapa nchini ninachokiheshimu hapa nchini kutokana na kuwa na waandishi wa habari waliobobea kwenye uandishi wa habari wakitamka bila woga na kwa kujiamini kabisa kuwa utaratibu wa malipo ulikuwa mzuri!!!!!!!!Jambo ambalo hata ukimwuliza mtu aliyetoka usingizini kuhusu utaratibu wa malipo hayo atakuambia ni ubabaishaji na wizi mtupu.
Tatizo ni kwamba mambo mengi hapa nchini yaendesheshwa kisiasa zaidi na kwa ajili ya manufaa ya watu wachache.Kwa mwenendo huu kweli wananchi watakuwa na imani na serikali yao???? Hivi hakuna njia kweli ambayo inaweza kufanyika zaidi ya kile kilichofanyika Mbagala kuhusu fidia ya waathirika hawa ambao ni watanzania wenzetu.
Serikali imetenga sh 8.5 bilioni kwa ajili ya kulipa fidia kwa watu walioathirika kwenye milipuko mabomu iliyojeruhi,kuathiri nyumba 9,000 na kuua zaidi ya watu 26,

Post a Comment