MTANGAZAJI

JANGIRI SUGU

Jangiri anayedaiwa kuwa ni sugu, Kaburu Yamungu Moshi (31) akiwa amefungwa pingu huku akiwa ameshikilia bundukia aina ya Riffle na nyama pembeni mara baada ya kukamatwa na askari wa wanyama pori katika kijiji cha Kidudwe wilaya ya Mvomero akidaiwa kuwinda wanyama bila ya kibali katika mbuga ya Wami-mbiki mkoa wa Morogoro na Pwani wakati alipofikishwa katika ofisi za Maliasili mkoani Morogoro

Askari wa wanyama pori katika mbuga ya Wami-Mbiki iliyopo mkoa wa Morogoro na Pwani Lucas Peter (kushoto) na Johari Ngwaji ( kulia) wakitoa nyama na vifaa vya Jangiri , Kaburu Yamungu Moshi (31).(picha zote na Juma Mtanda)

Askari wa Hifadhi ya Wanyama pori wa Wami Mbiki iliyopo kati ya Mkoa wa Pwani na Morogoro wamemtia mbaraoni mtu mmoja anayedaiwa kuwa jangili sugu Kaburu Yamungu Moshi (31) mkazi wa kijiji cha Kidudwe Kitongoji cha Sungwindala Wilaya Mvomero tarafa ya Turiani Mkoani hapa ambaye alikuwa akisakwa kwa tuhuma za kuendesha shughuli za uwindaji katika hifadhi hiyo kinyume cha sheria.
Akizungumzia tukio hilo kwa waandishi wa habari mkoani hapa Kaimu Meneja Mradi wa Hifadhi ya Wami Mbiki Aboubakari Msonde alisema kuwa tukio la kukamatwa kwa mtu huyo anayedaiwa kuwa ni jangili sugu lilitokea agosti 28 majira ya saa 11 alfajiri .
Alisema kuwa msako wa pamoja uliokuwa ukiongozwa na askari wa wanyama pori, askari wa jeshi la Polisi na wataalaam wa maliasili Mkoa wa Morogoro na baadhi ya viongozi wa Jumuiya waliokuwa wakiendesha operesheni dhidi ya ujangiri katika hifadhi walifanikiwa kumpita mbaroni mtu huyo ambaye anadaiwa kuwa raia wa nchi ya Burundi akiwa na nyama pori ya kuro na swala na bunduki aina riffle 375 na risasi tano.
Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na alamu na tochi kwa ajili ya kuwahadaa wanyama pori kabla ya kuwashambulia kwa risasi ambapo kabla ya kutiwa mbaroni alifanya jaribio ya kuwashambulia askari wa wanyama kabla ya kudhibitiwa na askari hao wa wanyama pori.
Msonde alisema kuwa jangili huyo ambaye tayari awali alikamatwa na kukabiliwa na kesi tatu tafauti mahakani alikuwa akisakwa kutokana kuendelea kuendesha vitendo vya uwindaji katika hifadhi hiyo bila ya kibali sambamba na wenzake ambao waliweza kutoroka kabla ya kutiwa mbaroni.
Aidha alisema kuwa baada ya kuhojiwa na maafisa wa Polisi na maliasili mkoani Morogoro na kukili kutenda tukio hilo pia Yamungu ambaye anadaiwa kuwa jangiri sugu katika hifadhi hiyo alibainika kuwa ni raia wa Burundi ambaye amekuwa akijihusisha na uwindaji haramu katika hifadhi hiyo kinyume na sheria za nchini licha ya kukabiliwa na kesi mbalimbali mahakamani.
Msonde alisema kuwa licha ya Yamungu kukabiliwa na kesi tatu tofauti mahakamani aliendelea kujihusisha na biashara haramu wa wanyama pori katika hifadhi ya Wami Mbiki na kutoa vitisho kwa raia na wafanyakazi wa hifadhi hiyo.
Naye Afisa Ardhi Maliasili na Mazingira Andengenye Malango alisema muundo wa sheria ya wanyama pori kifungu namba 12 ya mwaka 1974 mundo wake umepitwa na muda hivyo unehitaji marekebisho ya haraka licha ya kuwepo kwa sheria mpya ya mwaka 2009 ambayo utekelezaji wake bado haujaanza kutekelezeka hivyo ameiomba serikali kubasdilisha muunda iendane na wakati

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.