MTANGAZAJI

HII NDIO NDEGE ILIYOPATA AJALI LEO HUKO MBEYA


Ajali ya ndege namba 9J-BIO SESINA 206, imetokea leo asubuhi majira ya saa tatu eneo la Nanenane Uyole jijini Mbeya na abiria wanne wamenusurika kifo na hakuna aliyefariki.

Abiria walionusurika kifo ni pamoja JVER WAAK  (49) ambaye alikuwa Rubani, Raia wa Afrika Kusini, Bwana CHRISTIAN BASIL MMASI umri miaka 30, Ambaye ni Afisa Utawala wa mashamba ya Kapunga wilaya ya Mbarali, Balozi MOHAMMED RAMIA (64) mkazi wa Masaki jijini 
Dar es Salaam ambaye ni mfanyakazi wa EXPORT TRADING na Bwana SUNNY TAYIR (50) mfanyakazi wa EXPORT TRADING.

Chanzo cha ajali hiyo kinaelezwa kuwa ni hitilafu katika injini

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.